HabariNewsSiasa

RAISI MTEULE WILLIAM RUTO AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS ANAYEONDOKA UHURU KENYATTA.

Rais mteule William Ruto amesema amefanya mazungumzo na rais anayeondoka Uhuru Kenyatta kwa njia ya simu.

Kupitia ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter, Ruto amesema kwamba mazungumzo yao yamejikita zaidi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, na shughuli ya mpito inayotarajiwa kutoa madaraka kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta anayeondoka hadi kwa rais mteule William Ruto.

Mazungumzo haya yanafanyika siku mbili baada ya mahakama ya upeo kuhafiki ushundi wa Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

BY EDITORIAL DESK