HabariMombasaNewsSiasa

WAKAAZI WA MOMBASA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA GAVANA MTEULE ABDULSWAMAD SHARIFF NASSIR ILI KUFANIKISHA AJENDA YA MAENDELEO.

Msaidizi wa gavana mteule kaunti ya Mombasa Mahmoud Noor amewataka wakaazi wa Mombasa kushirikiana na gavana mteule AbdulSwamad Shariff Nassir ili kufanikisha ajenda ya maendeleo aliyowaahidi.

Akizungumza katika kipindi cha Sauti Asubuhi, Noor amedai kwamba mgao unaotoka kwa serikali kuu kuja kwa kaunti ni wa chini akidokeza kwamba ipo haja kwa Nassir, kuwa na ushirikiano na mashirika mbalimbali na wafadhili wa kimataifa kukidhi mahitaji mengi ya wakaazi.

Wakati uo huo amemtetea Nassir kwa madai ya kuwa kibaraka wa gavana anayeondoka Hassan Joho huku akipuuzilia mbali madai ya kutoafikiwa kwa maendeleo katika kaunti ya Mombasa kutokana na kuchaguliwa kwa Nassir kupitia mrengo pinzani wa Azimio.

Vilevile Noor amewataka wakaazi kudumisha usafi.

BY EDITORIAL DESK