HabariNewsSiasa

Kikao cha kuapisha wabunge watakaohudumu katika bunge la 13 kimefanyika leo.

Kikao cha kuapisha wabunge watakaohudumu katika bunge la 13 kimefanyika leo na kuongozwa na kaimu karani wa bunge hilo Sara Kioko.

katika taratibu wabunge walioshikilia nyadhifa bungeni katika mabunge ya awali wamepewa nafasi ya kwanza.

Katika orodha hiyo waliokuwa viongozi wa wengi na wachache Aden Duale na John Mbadi wamepata nafasi ya kwanza wakifuatwa na aliyewahi kuwa naibu spika Fara Maalim.

Karani huyo wa bunge Sara Kioko Alianza kwa kuwafahamisiha wabunge kuhusu umuhimu wa kula Kiapo, akiwasistizia kuwa kisheria hawawezi kutekeleza jukumu lolote kabla kuapishwa.

Wakati huo huo shughuli ya kuwaapisha maseneta wateule pia imekuwa ikiendelea chini ya uongozi wa karani wa seneti Jeremiah Nyegenye.

BY EDITORIAL DESK