HabariMazingiraMombasaNewsSiasa

Wadau wa maswala ya mazingira hapa pwani washinikiza serikali za kaunti Pamoja na serikali kuu kutafuta suluhu la kudumu kuhusu uchafuzi wa mazingira

Wakiongozwa na Daktari Mwinga Chokwe kutoka shirika la Clean Mombasa wanasema kutapakaa kwa taka sehemu mbali mbali mjini Mombasa kunafaa kuangaziwa kwa kina.

Chokwe amesema juhudi za kutunza mazingira zimepuuzwa na kuna haja ya serikali kuingilia kati kushirikiana na wadau hao ili kutatua tatizo hilo.

Kwa upande wao gavana mteule kaunti ya Mombasa Abdhulswamad Sharif nassir na naibu wake Francis Thoya wameapa kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa kero kwa muda sasa.

BY EDITORIAL DESK