HabariNewsSiasa

Naibu gavana Kaunti ya baringo Charles Kipng’ok ameaga dunia.

Naibu gavana Kaunti ya baringo Charles Kipng’ok ameaga dunia usiku wa kuamika leo akiwa safarini Kuja hapa Mombasa kutumia ndege ya shirika la Kenya Airways.

Gavana wa baringo Benjamin Cheboi amethibitisha Kifo cha Naibu Wake.

Awali shirika la ndege la Kenya Airways Ilituma taarifa kuhusu abiria kufariki, japo haikua imetoa Jina.

Shirika hilo limesema abiria huyo aliyekuwa akisafiri kutoka Nairibi Kuja Mombasa alikumbwa na matatizo ya kupumua kabla ya kufariki dunia akiwa katika uwanja wa JKIA akisubiri kuabiri Ndege.

Alikuwa ameratibiwa kupanda ndege saa moja usiku kuja hapa mjini Mombasa kuhudhuria mkutano wa Magavana.

Hiki ni kisa cha 3 cha abiria kufariki dunia akiwa katika ndege ya shirika hilo la Kenya airways katika siku za hivi karibuni.

BY EDITORIAL DESK