HabariMombasaNews

Afisa wa polisi eneo la Nyali hapa Mombasa apatikana akiwa amepoteza fahamu kwenye eneo la Leisure.

Afisa mmoja wa polisi eneo la Nyali hapa Mombasa amepatikana akiwa amepoteza fahamu kwenye eneo la Leisure mapema leo.

Inasemekana afisa huyo aliyekuwa zamu ya usiku ya kushika doria ameibiwa bunduki kabla ya kusafirishwa hadi eneo hilo.

Inakisiwa kuwa huenda waliomuibiwa walimpa dawa zilizomfanya kupoteza fahamu.

Tayari afisa huyo ameondolewa na kupelekwa katika hospitali moja ambako atafanyiwa uchunguzi wa Kiafya.

Idara ya Polisi imesema inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.

BY EDITORIAL DESK