FoodHabariNews

Wakulima kutoka kaunti ya Kwale wamehimizwa kuchagua mbegu sahihi watakazo panda msimu huu.

Wakulima kutoka kaunti ya Kwale wamehimizwa kuchagua mbegu sahihi watakazo panda msimu huu kwani utabiri unaonyesha hakuna mvua yakutosha hivyo tamaa ya kupata mavuno mazuri yapo lakini endapo wakulima watafuata utaratibu mzuri wa kilimo.

Mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya anga kwale Dominick Mbindyo, amewasihi waliokuwa wamechanganywa hali ya msimu huu na kukosa kutambua ni aina gani ya mbegu wanafaa kupanda.

Kauli hii inajiri baada ya wakulima wengi waliokuwa wamekata tamaa ya kushiriki kilimo msimu huu kutokana na kuwa na marasha rasha ya mvua tu hali ambayo imeathiri baadhi ya sehemu kukumbwa na kiangazi hapa kaunti ya Kwale.

Kwa upande wake afisaa wa kilimo eneo bunge la matuga, Kevin Makewa amewashauri wakulima kushiriki upanzi wa mbegu ambazo hazihitaji maji mengi kutoa mazao mazuri kwani wakati wa mvua chache mimea kama mahindi hayawezi kufanya vyema.

Aidha Makewa ameendelea kusema kuwa kuanzia mwezi oktoba mpaka disemba mkulima anaweza kushiriki upanzi wa mimea inayohitaji maji kidogo kama mtama na mbegu zengine isipokuwa mahindi.

BY EDITORIAL DESK