HabariNews

Pendekezo limetolewa kwa ngazi zote za serikali kuidhinisha mpango wa kusambaza sodo katika shule za msingi na sekondari.

Pendekezo limetolewa kwa ngazi zote za serikali kuidhinisha mpango wa kusambaza sodo katika shule za msingi na sekondari katika kaunti ya kwale hususan watoto wanaotoka sehemu kame.

Akizungumza na wanahabari afisaa wa afya kutoka shirika la Adis Clinic Caroline Wanjiru amesema kuwa usambazaji huo utapunguza visa wa wanafunzi wa kike kukosa masomo Nyakati za heidh.

Kulingana na afisaa huyo wasichana wengi kutoka jamii zisizojiweza hususan Kinango na eneo bunge la lungalunga wameacha shule kutokana na ukosefu wa sodo .

Wakati uo huo ameitaja hali hiyo imechangia pakubwa kwa baadhi ya wasichana kuingia katika ndoa za Mapema pamoja na kuajiriwa ili kuwasaidia wazazi na majukumu ya nyumbani hali ambayo ni kinyume na Sheria za watoto.

BY EDITORIAL DESK