HabariNewsSiasa

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewatahadharisha wananchi dhidi ya uuzaji ardhi zao kiholela.

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewatahadharisha wananchi dhidi ya uuzaji ardhi zao kiholela akisema hiyo imechangia migogoro mingi ya ardhi inayoshuhudiwa katika Kaunti hiyo.

Akizungumzia tukio la hivi majuzi katika eneo la Mwembeni Wadi ya Samburu/Chengoni ambapo zaidi ya familia 25 ziliachwa bila makao baada ya nyumba zao kubomolewa na kutekelezwa na genge la watu waliokuwa wamejihami, Achani amesema ardhi ni raslimali muhimu inayofaa kuchungwa.

Huku hayo yakijiri, Achani vilevile amewataka Wazazi kaunti ya Kwale kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya mimba na ndoa za mapema miongoni mwa wasichana.

Akizungumza katika eneo bunge la Samburu gavana wa Kwale Fatuma Achani amewahimiza wazazi kupambana na visa vya ndoa na mimba za mapema hususan wasichana walio chini ya umri wa miaka 18.

Aidha kiongozi huyo amevitaja visa hivyo viwili kama vyanzo kikuu cha kuzorota kwa viwango wa elimu ya watoto wa kike katika jamii.

BY EDITORIAL DESK