AfyaHabariNews

Idadi ya watu wanaougua saratani kaunti ya Kwale inazidi kuongezeka.

Idadi ya watu wanaougua saratani kaunti ya Kwale inazidi kuongezeka baada ya watu 80 kupatikana na ugonjwa huo mwaka huu.

Haya ni kwa mujibu wa gavana wa Kwale Fatuma Achani anayesema kuwa takriban visa 200 vya wagonjwa wa saratani vimeripotiwa kaunti hiyo.

Akizungumza katika eneo la Samburu, Achani amewataka wakaazi kujitokeza kwa wingi kupimwa saratani ili waweze kutambua hali zao mapema.

Wakati uo huo, Achani amewahakikishia wakaazi kuwa kituo cha saratani kinachojengwa kaunti hiyo kitakamilika hivi karibuni ili wagonjwa wasitaabike kutafuta huduma za matibabu ya ugonjwa huo.

Gavana huyo ameyasema hayo baada ya kufanya matembezi ya kuihamasisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani katika eneo hilo.

BY EDITORIAL DESK