HabariNews

WATU WATATU WAAGA DUNIA BAADA YA KUHUSIKA KATIKA AJALI MBAYA.

Watu watatu wameaga dunia baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani mapema leo katika eneo la Kijipwa eneo bunge la Kilifi kusini.

Akithibitisha ajali hiyo kamanda wa polisi eneo la Kilifi kusini Mohamed Wako ameeleza kuwa ajali hiyo iliyohusisha piki piki mbili imesababisha waendeshaji wa pikipiki hizo kupotezayao papo hapo, huku msichana mmoja aliyekuwa ni abiria katika moja ya pikipiki hizo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitalini.

Kulingana na kamanda huyo piki piki hizo zilikua zimewabeba wasichana wawili wakielekea shuleni na abiria mmoja ambapo kwa sasa wawili hao wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa kaunti ya Kilifi.

Wakati huo huo Wako ametoa wito kwa waendeshaji pikipiki kuwa waangalifu barabarani na vile vile akawasistiza kuhudhuria mafunzo ya uendeshaji pikipiki ili kuzuia ajali kama hizi kutokea.

BY EDITORIAL DESK