HabariNewsSiasa

Viongozi waliochaguliwa katika kaunti ya Kwale watakiwa kushirikiana na vijana.

Wito watolewa kwa viongozi wa kisiasa waliochaguliwa kaunti ya Kwale kushirikiana na vijana ili kutatua changamoto ya utovu wa usalama katika jamii

Kulingana na mkurugenzi wa Shirika la kijamii la Kwale Focus Mesalimu Rambo, ushirikiano huo unalenga kuhakikisha vijana wanaishi kwa umoja na uwiano baada ya kipindi cha uchaguzi kukamilika.

Akizungumza katika eneo la Kiteje katika wadi ya Waa/Ng’ombeni, Rambo amesema pia wanalenga kukuza vipaji vya vijana kupitia mradi wa kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha amani kupitia michezo.

Kwa upande wake mwakilishi wa kike kaunti hii Fatuma Masito ameahidi kushirikiana na shirika hilo ili kukabiliana na visa vya uhalifu vilivyokithiri katika eneo hilo.

Masito amesema kuwa analenga kutumia mgao wa bajeti ya hazina ya NGAAF ili kuwawezesha vijana kujiendeleza kimaisha.

BY EDITORIAL DESK