HabariMombasaNews

WITO WATOLEWA KWA GAVANA ABDUL SWAMAD SHARIFF NASSIR KUFANYA MAZUNGUMZO NA BAADHI YA MAAFISA WA KAUNTI.

Wito umetolewa kwa gavana wa Mombasa Abdul Swamad Shariff Nassir kufanya mazungumzo na baadhi ya maafisa wa kaunti wanaodaiwa kuwahangaisha wafanyabiashara wadogo wadogo katika shugli zao.

Wafanya biashara wamelalamikia kuhangaishwa na baadhi ya maafisa wa kaunti wanaodaiwa kuwapokonywa vyombo na bidha zao za biashara kabla ya kuwatozwa pesa ili kukomboa mali hizo. Hali ambayo wamesema inawalemaza katika biashara zao.

Wafanya biashara hao wamemtaka gavana wa Mombasa kutoa amri itakayoleta afueni kwao kupata mazingira bora ya kujiendeleza katika bishara zao.

BY EDITORIAL DESK