HabariNewsSiasa

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MASHUJAA ZAENDELEA KATIKA BUSTANI LA UHURU JIJINI NAIROBI.

Raisi William Ruto anawaongoza viongozi mbalimbali na wakenya katika maadhimisho ya sherehe za mashujaa katika bustani ya uhuru jijini Nairobi.

Aidha naibu wa rais Rigathi Gachagua amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliokamilika akiwataka kuwajibika kazini.

Kwa upande wake gavana wa jimbo la Nairobi Johnson Sakaja amewapongeza wakenya kwa kudumisha amani wakti na baada ya uchaguzi akiwataja kama mashujaa.

Maadhimisho hayo ni ya 59 tangu Kenya kujinyakulia uhuru mwaka 1964 bada ya mapambano makali na serikali ya mkoloni, mashuja kadhaa wakitarajiwa kutambuliwa na raisi William Ruto.

BY EDITORIAL DESK