HabariNewsSiasa

Serikali ya kaunti ya Kwale imewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo watakomesha unyakuzi wa ardhi.

Serikali ya kaunti ya Kwale imewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo watakomesha unyakuzi wa ardhi unaoshuhudiwa kwa sasa.

Akizungumza mjini Kwale Gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema kuwa serikali iliyoko mamlakani iko tayari kukabiliana na mabwenyenye ambao wanapokonya wakaazi wa Kwale mashamba yao kiholela.

Aidha Achani amesema kuwa serikali ya kitaifa ikiongozwa na daktari William Ruto inajizatiti kukabiliana na wizi wa mashamba ambao umekithiri hususan eneo la Pwani.

Kauli yake inajiri baada ya mabwenyenye wanaodai kununua kipande cha ardhi kuvamia watu katika eneo la Mwembeni Samburu hatua iliyoacha Zaidi ya familia 25 bila makao baada ya nyumba zao kuchomwa nyakati za usiku.

BY EDITORIAL DESK