Habari

Shirika la msalaba mwekundu limetaja kupungua kwa asiliamia chache katika msambao wa virusi vya HIV ukanda wa pwani.

Shirika la msalaba mwekundu katika ukanda wa pwani limetaja kupungua kwa asiliamia chache katika msambao wa virusi vya HIV ukanda wa pwani hasa kaunti ya Mombasa baada ya juhudi zao za kupunguza msambao wa virusi hivyo kuanza kuzaa matunda.

Kwenye mazungumzo na vyombo vya habari hapa kaunti ya Mombasa afisa wa mipango katika shirika hilo ukanda wa pwani Msalam Ahmed amesema kuwa kufikia sasa shirika hilo kwa ushirikiano na mashirika mengine limeweza kudhiti unyanyapa miongoni mwa waathiriwa Pamoja na kupunguza idadi ya wanaoambukizwa ugonjwa huo katika kaunti ya Mombasa na pwani kwa jumla.

Kadhalika Msalam amesema kuwa mradi huo wa kudhiti msambao huo na dhulma kwa walengwa umegharimu shilingi Bilioni 1 kutoka julai 2021 na unatarajia kukamilika juni 2024.

Kwa upande wa shirika la reach out center ambalo ni mshika dau mkuu katika ajenda ya kudhibiti matumizi ya madawa za kulevya kwa vijana na waathiriwa kupitia msimamizi wake Taib Abdulrahman limetoa pongeza kwa wadau wa maswala ya sheria ambao wamejitokeza kufanikisha juhudi hizo za kutetea walengwa katika harakati za kufahamu hazi zao.

Wakili Titus mnyoki kwa upande ameyaomba mashirika hayo kuzingatia pakubwa ushirikiano na chama cha mawakili nchini LSK ili kuweza kutoa msaada kwa waathiriwa ambao hawana uwezo.

Mashirika haya yalikuja Pamoja katika hafla ya kutoa mafunzo kwa wadau wa sheria kutoka kaunti zote sita za pwani lengo kuu ni kuondoa unyanyapaa miongoni mwa walengwa na kutoa hamasa kwa jamii kuhusu haki za waathiriwa wadhamini wakuu liiwa ni shirika la msalaba mwekundi kupitia Global fund.

BY DAVID OTIENO