HabariNewsSiasa

Viongozi wa kike kaunti ya Kwale sasa wanataka kuhuhusishwa kikamilifu katika maswala ya ardhi na madini.

Viongozi wa kike kaunti ya Kwale sasa wanamtaka waziri mpya wa madini Salim Mvurya kuhakikisha wanawake wanahusishwa kikamilifu katika maswala ya ardhi na madini.

Wakiongozwa na aliyekuwa mgombea wa kiti cha wadi ya Ukunda Hawa Salim na mwenzake Gladys Mwakisha, viongozi hao wamemtaka Mvurya kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele katika umiliki wa ardhi na uchimbaji wa madini.

Wakizungumza na wanahabari katika eneo hilo, wanawake hao wamemtaka pia Mvurya kuangazia suala la ulipaji wa fidia ili wakaazi walioathirika na shughuli za uchimbaji madini waweze kufaidika.

Kwa upande wao viongozi wa kiume wamemtaka Mvurya kuhakikisha waathiriwa wanapata mgao wa fedha za uchimbaji wa madini unaoendelezwa na kampuni ya Base Titanium.

Wakiongozwa na aliyekuwa mgombea na kiti cha ubunge wa Msambweni Peter Nzuki, viongozi hao wamesema kucheleweshwa kwa fedha hizo kumeathiri uchumi wa kaunti hiyo.

BY EDITORIAL DESK