HabariNews

Serikali ya kitaifa imetakiwa kuimarisha usalama kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi.

Serikali ya kitaifa imetakiwa kuimarisha usalama kaunti ndogo ya Magarini kaunti ya Kilifi ili kumaliza visa vya wanafunzi kuvamiwa wakiwa njiani kuelekea shuleni.

Kulingana na wakaazi eneo hilo wakiongozwa na John Kombe, kwa sasa wafanyibiashara wanaathirika pakubwa na utovu wa usalama.

Kombe amependekeza kujengwa kwa kituo cha polisi ili kuimarisha usalama hata zaidi.

Wakati uohuo wakaazi hao wamewaonya makundi ya vijana wanaowashambulia wanafunzi pamoja na wakaazi kuwa watakabiliwa na wenyeji.

Wenyeji hao wanasema kuwa wanawafahamu vijana wanaotekeleza uhalifu na wakawaonya vikali dhidi ya kuendesha vitendo hivyo.

BY EDITORIAL DESK