HabariMombasaNewsSiasa

Gavana wa Mombasa Abdhulswamad Nassir aahidi kulipa mishahara ya wafanyakazi kaunti ya Mombasa.

Mgomo wa muungano wa madaktari hapa Mombasa uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Ijumaa wiki hii huenda ukastishwa.

Hii ni baada ya gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kuahidi kuwalipa misharaha wafanyikazi wote wa kaunti wakiwemo wahudumu wa afya.

Akizungumza ofisini mwake mapema leo gavana Nassir amesema kuwa pesa za kushughulikia mishahara ya wafanyikazi wa kaunti ya Mombasa tayari zimeingia kwa Akaunti husika.

Hata hivyo amewaomba wafanyikazi hao kutekeleza majukumu yao ya kazi za huduma kwa wananchi.

Nassir amedokeza kuwa alirithi serikali ikiwa katika hali mbaya, ikiwemo kuwa na upungufu wa fedha hali ambayo imechangia pakubwa katika kutekeleza haki za wafanyikazi.

BY EDITORIAL DESK