HabariMombasaNews

Madereva wa texi Mombasa wapongeza hatua ya marubani wa KQ kusitisha mgomo.

Madereva wa texi katika kaunti ya Mombasa wameeleza furaha yao baada ya mahakama ya leba kuamuru marubani wa ndege wa shirika la ndege la kenya air ways kurejea kazini kuanzia leo alfajiri

Akizumgumza na meza yetu ya habari mmoja wa dereva hao John Wambogo amesema kuwa wamepokea tangazo hilo kwa furaha kwa kuwa tegemeo lao kubwa ni abiria wanao safiri kwa kutumia ndege.

Ameongezea kuwa wanatarajia kufaidi zaidi hasa tunapoelekea msimu wa krismasi na mwaka mpya ambapo watalii zaidi kutoka nchi za nje wanatarajiwa kuja hapa nchini

baadhi yao wasema kuwa hawajathirika pakubwa na mgomo wao kwa vile wamekuwa na njia tofauti na kusafirisha abiria hadi uwanja wa ndege wakati huo wa mgomo wa marubani.

Hata hivyo madereva wamesema wanahofu iwapo mgomo huo ungeendelea kenya ingepoteza watalii zaidi ambao huenda wangetembelea mataifa mengine barani afrika.

BY EDITORIAL TEAM