HabariNews

Sekta ya utalii katika eneo la Diani kaunti ya Kwale inatarajiwa kuimarika.

Sekta ya utalii katika eneo la Diani kaunti ya Kwale inatarajiwa kuimarika msimu huu wa sherehe za krismasi kufuatia ongezeko la idadi ya wageni.

Washikadau wa sekta hiyo wameitaka serikali ya kaunti kuimarisha hali ya usalama baada ya hoteli za kitalii za eneo hilo kurekodi asilimia 80 ya wageni wa kimataifa na wa humu nchini.

Wakiongozwa na meneja wa hoteli ya kitalii ya Jacaranda Jacob Kirori na mwenzake wa Swahili Jaob Andayi, washikadau hao wameitaka serikali kuweka mataa ya kutosha barabarani ili kuimarisha usalama nyakati za usiku.

Kwa upande wao baadhi ya watalii waliozuru fuo za bahari za Diani wameelezea kufurahishwa na mandhari mazuri ya eneo hilo.

Wakiongozwa na Juliash Anubi, wageni hao wametaka idadi ya maafisa wa polisi wanaoshika doria usiku kuongezwa ili kuboresha usalama.

BY NEWS DESK