HabariNews

KERRA yaweka mikakati ya kuimarisha ujenzi wa barabara vijijini.

Mamlaka ya usimamizi wa barabara za mashinani (KERRA) imeweka mikakati ya kuimarisha ujenzi wa barabara za vijijini ili kuzuia visa vya ajali miongoni mwa wahudumu wa bodaboda.

Mhandisi wa mamlaka hiyo kaunti ya Kwale Onesmus Ikua amesema kuwa tayari wameanzisha ukarabati wa barabara ya Jacaranda-Diani inayotarajiwa kuwekwa alama za barabara.

Haya yanajiri baada ya wahudumu hao kulalamikia ukosefu wa alama za barabarani zinazochangia pakubwa ajali za waendeshaji pikipiki.

Kwa upande wake Mhandisi wa mamlaka ya usimamizi wa barabara kuu nchini (KeNHA) Peter Maruti amelalamikia ongezeko la visa vya uharibifu wa alama za barabarani.

Maruti sasa anawataka wahudumu wa bodaboda kuripoti visa hivyo kwa polisi ili washukiwa waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

BY EDITORIAL TEAM