HabariNews

Polisi katika kaunti ya kwale watakiwa kutoingilia maswala ya umiliki wa ardhi.

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka maafisa wa polisi kaunti hiyo kutoingilia maswala ya umiliki wa ardhi katika eneo la Shimoni.

Akizngumza katika eneo hilo, Achani amedai kuwa baadhi ya maafisa hao wamekuwa wakitumiwa vibaya na mabwenyenye kuwadhulumu wenyeji mashamba yao.

Gavana huyo amemtaka kamishna wa Kwale Gideon Oyagi kuhakikisha maafisa wake hawajihusishi na maswala ya unyakuzi wa ardhi za wakaazi.

Ni kauli iliyoungwa mkono na mbunge wa Lungalunga Mangale Chiforomodo anayeitaka tume ya kitaifa ya ardhi (NLC) kutatua mizozo ya ardhi katika eneo hilo.

Chiforomodo amesema kuwa tayari ameanzisha juhudi za kuhakikisha wenyeji wanapata haki ya ardhi zao.

BY EDITORIAL TEAM.