HabariNews

Serikali ya kitaifa inalenga kuanzisha mikakati ya kuboresha sekta ya uvuvi.

Serikali ya kitaifa inalenga kuanzisha mikakati ya kuboresha sekta ya uvuvi ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki nchini.

Waziri wa maswala ya uchumi wa bahari Salim Mvurya amesema kuwa serikali inanuia kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo ili kuongeza kiwango cha mapato yao.

Akizungumza huko Shimoni kaunti ya Kwale, Mvurya amesisitiza haja ya kuongeza asilimia 17 ya mapato ya uvuvi nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa maswala ya uvuvi na bahari (KMFRI) Profesa James Njiru amesema ukosefu wa mbegu zilizoidhinishwa na watalaam umechangia uhaba wa samaki nchini.

Njiru amedokeza kwamba taasisi hiyo imeanzisha mradi wa ufugaji wa samaki katika eneo hilo ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki.

BY EDITORIAL DESK