HabariNews

Wakaazi wa Kwale waombwa kupokea chanjo dhidi ya Corona.

Wizara ya afya na ile ya usalama kaunti ya kwale imewahimiza wakaazi kujitokeza na kupokea chanjo dhidi ya Corona kabla ya kukamilika kwa zoezi hilo mwezi ujao kote nchini.

Hii ni baada ya kubainika kwamba ni asilimia 18.2 pekee ya wakaazi waliopata chanjo tangu kuanza kwa zoezi hilo humu nchini licha ya kaunti hio kuendelea kurekodi visa vya maambukizi ya Corona.

Msaidizi wa kamishna wa Kwale Timothy Omoit na mshirikishi wa chanjo Edward Mumbo wameitaja idadi hio kuwa ya chini mno wakisema kwamba kampeni za kuhamasisha jamii zimeanzishwa umuhimu wa chanjo dhidi ya Corona imeanzishwa.

Zoezi hilo linalenga watoto elfu 152 wenye miaka 12 hadi 17 baada ya kubainika kuwa ni asilimia 2 pekee ya watoto hao waliopata chanjo hio.

BY EDITORIAL TEAM