HabariNews

Maafisa wa usalama baharini wa Coast guard watakiwa kukoma kuwahangaisha wavuvi katika eneo la Shimoni.

Onyo latolewa na Mwakilishi wa kike kaunti ya Kwale Fatuma Masito dhidi ya maafisa wa usalama baharini wa Coast guard kukoma kuwahangaisha wavuvi katika eneo la Shimoni.

Akizungumza huku Shimoni wadi ya Vanga, kiongozi huyo amewataka maafisa wanaoshika doria kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ili usalama wa wavuvi uwezi kupatikana wala sio kuwahangaisha.

Kwa uapnde wake afisaa msimamizi wa maafisa hao kutoka eneo hilo John Ogongi amekanusha madai hayo na kusema kwamba wao kama maafisa wa usalama baharini wanafanya majukumu yao kwa kuzingatia sheria.

BY EDITORIAL TEAM