HabariNews

Shirika la samba sports youth ajenda limezindua mchezo wa kuigiza maarufu VAR call.

Shirika la samba sports youth ajenda limezindua mchezo wa kuigiza maarufu VAR call, mchezo unaoangazia madhila anayopitia mtoto wa kike katika jamii ikiwemo masuala ya dhulma za kijinsia.

Mshirikishi wa shirika hilo Mohammed Mwachausa ametaja uzinduzi huo kuwa kati ya jitihada za shirika hilo kushirikiana na idara mbalimbali zinazoangazia maslahi ya mtoto wa kike katika kukabiliana na changamoto anazopitia mtoto wa kike katika jamii.

Mwachausa amesema changamoto hizo zimekua zikiathiri maisha ya mtoto wa kike kwa ujumla huku wengine wakilazimika kusitisha masomo kutokana na kupachikwa mimba za mapema kati ya madhila mengine mengi.

Amesema tayari wameweza kuwafikia watoto takriban elfu 30 pamoja na wazazi zaidi ya elfu sita katika magatuzi yote ya kaunti ya Kwale kupitia hamasa katika kukabiliana na changamoto zinazomkumba hususan mtoto wa kike katika jamii.

Hata hivyo amesema shirika hilo limeweka mikakati zaidi ya kuongeza jitihada zake katika kuboresha maisha katika jamii kwa kuhakikisha mila na dhana potofu zinatokomezwa.

BY EDITORIAL TEAM