HabariNews

Jamii ya Wamakonde yawaonya viongozi kutoka taifa la Msumbiji dhidi ya kuwashawishi kuwapigia kura.

Jamii ya Wamakonde inayoishi katika eneo la Makongeni kaunti ya Kwale imewaonya viongozi kutoka taifa la Msumbiji dhidi ya kuwashawishi kuwapigia kura.

Mwenyekiti wa jamii hiyo Thomas Nguli amesisitiza kuwa ni raia wa Kenya baada ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuwapa vitambulisho vya kitaifa mwaka wa 2016.

Jamii hiyo iliyowasili humu nchini zaidi ya miaka 50 iliyopita kufanya kazi katika mashamba ya makonge imewataka viongozi kutoka Msumbiji kutowashinikiza kushiriki kwenye chaguzi za taifa hilo.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kimataifa la chakula duniani (FAO) Carla Mucavi ameitaka jamii hiyo kujiunga kwa makundi ya wanawake na vijana ili kufaidika na miradi ya serikali.

Mucavi ambaye ni raia wa Msumbiji alikuwa ameandamana na naibu gavana wa kaunti hiyo Chirema Kombo aliyewataka wazazi kutilia maanani suala la elimu kwa wanao.

BY EDITORIAL DESK