HabariNews

Wafungwa 3 kutoka gereza la wanaume la Kwale ni miongoni mwa watahiniwa 50,407 mwaka huu 2022 ndani ya kaunti ya Kwale.

Wafungwa 3 kutoka gereza la wanaume la Kwale ni miongoni mwa watahiniwa 50,407 mwaka huu 2022 ndani ya kaunti ya Kwale.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa kasha la mitihani Kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amedokeza kuwa wafungwa hao wataweza kufanya mtihani wao katika gereza hilo ambapo mazingira salama yamewekwa ili kuwawezesha kufanya mtihani huo bila budha yoyote.

Aidha Oyagi ameendelea kusema kuwa kuna watahiniwa 10 ambao wanakalia mtihani wa watu wazima.

Wakati huo huo kamishna huyo amesema jumla ya wasichana elfu 11,248 wa shule za msingi watakalia mtihani wa kcpe na wasichana 878 wa shule za kibinafsi.

Huku Wavulana elfu 11,383 wakikalia mtihani wa kcpe katika shule za umma na wavulana 896 wa shule za kibinafsi.

Maafisa wa polisi 988 watasimamia mtihani huo mpaka utakapo kamilika.

Huku hayo yakijiri, Onyo Kali latolewa Kwa watakao jihusisha na udanganyifu wa mtihani kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Haya ni kulingana na kamishna wa Kwale Gideon Oyagi akisema kuwa idara ya usalama pamoja na asasi zote za usalama wanashirikiana kuona kwamba hakuna visa vyovyote vya udanganyifu vikavyo ripotiwa kutoka kaunti ya Kwale.

Aidha Oyagi anasema kufikia sasa hakuna visa vyovyote vilivyoripotiwa vitakavyo athiri matokea ya mtihani huo.

BY EDITORIAL TEAM