HabariNews

Baraza la magavana limesema kuwa halitatia sahihi mkataba wa vifaa vya afya almaarufu kama MES.

Baraza la magavana limesema kuwa halitatia sahihi mkataba wa vifaa vya afya almaarufu kama MES baada ya mkataba huo na wasambazaji wa vifaa hivyo kutamatika hadi pale matakwa yao yatakapotimizwa.

Akizungumza katika eneo la Diani kaunti ya Kwale baada ya kamati ya afya katika baraza la magavana kukutana mwenyekiti wa kamati hiyo Muthomi Njuki amesema kuwa mkataba wa kupewa vifaa hivyo umeleta athari zaidi ya faida zilizokusudiwa.

Akiongeza kuwa baadhi ya masharti ni lazima yaangaziwe upya na baraza hilo la sivyo hawatatia sahihi mkataba mpya.

Njuki ambaye pia ni gavana wa Tharaka Nithi amesema kuwa kaunti zitatia sahihi mkataba mpya wa miaka mitatu pale tu matakwa yao yatakapokubaliana na ya kampuni zinazosambaza vifaa hivyo.

Kwa upande wake waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema kuwa watafanya kazi na serikali za kaunti kuona kuwa vifaa hivyo na mikataba iliyopo inaangaziwa ili kumfaidi mwananchi.

BY EDITORIAL TEAM