HabariNews

Serikali ya kaunti ya Kwale imeweka mikakati ya kuwalinda wanawake wanaojihusisha na biashara dhidi ya dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo.

Serikali ya kaunti ya Kwale imeweka mikakati ya kuwalinda wanawake wanaojihusisha na biashara dhidi ya dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo.

Kwa mujibu wa afisa wa serikali ya kaunti kitengo cha ukaguzi Douglas Oginda, askari wa kutosha wa kaunti wamepelekwa kushika doria katika masoko ili kutoa ulinzi kwa wafanyibiashara wanawake.

Akizungumza katika kikao kilichoandaliwa na baraza la kitaifa la makanisa nchini (NCCK) kujadili usalama wa wanawake mjini Kwale, Oginda amesema kuwa hatua hiyo itahakikisha wanawake hawadhulumiwi wakati wanapoendeleza shughuli zao sokoni.

Kwa upande wake mwakilishi wa wanawake katika baraza hilo Eda Wamboi amewahimiza wanawake kaunti hiyo kuanzisha biashara zao ili wajiendeleze kimaisha.

BY EDITORIAL TEAM