HabariNews

Eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale limetajwa kuongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale limetajwa kuongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi katika kaunti hiyo.

Kulingana na waziri wa afya kaunti hiyo Francis Gwama, eneo hilo lenye mchanganyiko wa watu hasa katika mji wa kitalii wa Diani linaongoza kwa asilimia 4.8 ya maambukizi ya Ukimwi.

Gwama amesema kuwa Kwale iko na asilimia 3.2 ya maambukizi ya ugonjwa huo ikilinganishwa na asilimia 4.3 ya kitaifa.

Haya yanajiri huku maambukizi mapya ya ugonjwa huo yakitajwa kuchangiwa na vijana wanaoshiriki ngono ya mapema.

Afisa kutoka shirika la Maisha Youth Kenya Fauziah Wanguche amewataka vijana kutembelea vituo vya afya ili wapimwe na kujua hali zao.

BY EDITORIAL TEAM