HabariNews

Wito umetolewa kwa wananchi katika eneo la Lungalunga kujitokeza kuchukua vitambulisho vya kitaifa.

Wito umetolewa kwa wananchi waliofikisha miaka 18 na zaidi katika eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale kuhakikisha wanajitokeza kuchukua vitambulisho vya kitaifa.

Kulingana na Naibu kamishna wa eneo hilo Joseph Sawe amesema kuwa baadhi ya wananchi hawatilii maanani umiliki wa stakabadhi hiyo muhimu mpaka pale wanapofikwa na majanga.

Sawe ameendelea kusema kuwa wengi wao hukosa kupata huduma muhimu za serikali kwa ukosefu wa stakabadhi hiyo na mwishowe kulaumu serikali.

Haya yanajiri baada ya baadhi ya wananchi katika wadi ya Mwereni , Lungalunga wanaodai kuvamiwa na ndovu kukosa kulipwa fidia zao kwa kukosa vitambulisho.

BY EDITORIAL DESK