HabariNews

Viongozi katika kaunti ya Kwale wameapa kushirikiana ili kukabiliana na tatizo la njaa.

Viongozi katika kaunti ya Kwale wameapa kushirikiana ili kukabiliana na tatizo la njaa linaloshuhudiwa katika kaunti hiyo.

Wakiongozwa na mbunge wa Lungalunga Mangale Chiforomodo viongozi hao wamesema kuwa kuna umuhimu wa kuhimiza wananchi tamaduni ya kutoa kwa majirani zao.

Chiforomodo akisema kuwa swala la baa la njaa linahitaji ushirikiano ili kukabiliana nalo.

Ni jambo lililoungwa mkono na mwenzake wa Matuga Kassim Tandaza ambaye amesema kuwa viongozi wanapowajibika kwa pamoja maswala mengi hupata suluhu ya haraka.

Kwa upande wake mwakilishi wa wanawake kaunti hiyo Fatuma Masito bidii ya viongozi husaidia kwani baadhi ya sehemu zinakabiliwa na tatizo hilo kwa muda sasa.

BY EDITORIAL DESK