AfyaHabariNews

Viongozi wa kidini kaunti ya Kwale sasa wanahofu kuwa huenda viwango vya maambukizi ya virusi vya corona vikaongezeka ifikapo Januari mwaka ujao.

Viongozi wa kidini kaunti ya Kwale sasa wanahofu kuwa huenda viwango vya maambukizi ya virusi vya corona vikaongezeka ifikapo Januari mwaka ujao.

Meneja wa mipango katika baraza la muungano wa viongozi hao (IRCK) Linus Nthigai anahofia kuongezeka kwa maambukizi hayo kufuatia idadi kubwa ya wageni wanaozuru eneo la Pwani.

Nthigai amesema kuwa viongozi hao watashirikiana na wizara ya afya kaunti hiyo ili kuwahamasisha na kuwachanja wananchi katika maeneo ya ibada baada ya shamrashamra za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wake muuguzi msimamizi katika hospitali ya Diani Grace Thumbi amesema kuwa ushirikiano huo utarahisisha pakubwa shughuli ya utoaji chanjo.

Hata hivyo, Thumbi amedokeza kwamba idadi ya wakaazi wanaojitokeza kudungwa chanjo ya corona ingali iko ndogo kaunti hiyo.

BY EDITORIAL DESK