HabariNews

Wakaazi wa Kasemeni wanalalamikia kutengwa katika nafasi za ajira za mradi wa bwawa la Mwache.

Wakaazi wa Kasemeni katika eneo la Mazeras huko Samburu kaunti ya Kwale wanalalamikia kutengwa katika nafasi za ajira za mradi wa bwawa la Mwache unaolenga kukabiliana na ukosefu wa maji katika eneo hilo.

Wakiongozwa na Christine Mbeka, wakaazi hao wamedai kuwa wasimamizi wa mradi huo wamekiuka makubaliano ya uajiri ambapo wenyeji walistahili kupewa kipaumbele.

Sasa wanasema kuwa mradi huo utakaogharimu takriban shilingi bilioni 20 umeingizwa ufisadi kwani idadi kubwa ya watu walioajiriwa ni wageni licha ya kuahidiwa kupatiwa asilimia 70 ya ajira.

Kwa upande wake afisa wa shirika la Transparency International kutoka kaunti ya Mombasa Brian Kibira amethibitisha kupokea malalamishi ya wakaazi hao.

Kibira ameahidi kuwa shirika hilo litatoa msaada wa kisheria kwa wakaazi walioathirika ili kukabiliana na visa vya ufisadi katika mradi huo.

BY EDITORIAL TEAM