HabariNews

Gavana wa kaunti ya Lamu issa Timamy amesema ako tayari kuwanunulia polisi mbwa wa kunusa ili waweze kukabiliana na suala sugu la mihadarati.

Gavana wa kaunti ya Lamu issa Timamy amesema ako tayari kuwanunulia polisi mbwa wa kunusa ili waweze kukabiliana na suala sugu la mihadarati.

Timamy aidha amewataka polisi kumkamata yeyote ambaye atafika katika kituo cha polisi kutaka kumkomboa mtu yeyote aliyekamatwa kwa shutuma za mihadarati akisema mtu huyo pia ni mshukiwa.

Naye Kamishena katika kaunti ya Lamu Irungu Macharia amewataka wananchi kushirikiana na polisi ili kufanikisha juhudi za polisi za kupambana na mihadarati.

Kwa upande wake, mbunge wa eneo bunge la Lamu Mashariki Ruweida Mohamed amewapongeza maafisa wa polisi kutoka eneo la Kizingitini kwa juhudi zao za kukabiliana na walanguzi wa mihadarati.

Mohamed amewataka viongozi kushirikiana kumaliza suala sugu la mihadarati kaunti ya Lamu.

BY EDITORIAL TEAM