HabariNews

Sekta ya utalii inatarajiwa kuimarika kwa kiwango kikubwa msimu huu.

Sekta ya utalii katika eneo la Diani kaunti ya Kwale inatarajiwa kuimarika kwa kiwango kikubwa wakati huu wa msimu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kulingana na mkurugenzi wa wahudumu wa mahoteli kusini mwa Pwani Sam Ikwaye amedokeza kuwa sekta hiyo inatarajiwa kuimarika zaidi kwa asilimia 90 huku wakipokea wageni kutoka ng’ambo na pia wageni wa humu nchini.

Aidha Ikwaye amesema kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha idadi ya wageni inaongezeka katika hoteli hizo wakati wa sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Wakati uo huo Mkurugenzi wa hoteli ya Baobab Jeff Mkolwe amesema kwamba sekta ya utalii eneo hilo inategemea pakubwa wageni wanaotoka humu nchini na nchi za kigeni unaosaidia kukuza utalii kwa ujumla.

Meneja huyo ameelezea kuwa tatizo la usafiri limeathiri pakubwa utalii wa kimataifa kutokana na janga la corona miaka miwili iliyopita.

BY EDITORIAL DESK