HabariNews

Mbunge wa Kinango Gonzi Rai amewahakikishia wakaazi wa Kinango kuwa wataendelea kupokea chakula cha msaada.

Mbunge wa Kinango Gonzi Rai amewahakikishia wakaazi wa Kinango kuwa wataendelea kupokea chakula cha msaada kufuatia baa la njaa linaloshuhudiwa katika eneo hilo.

Akiongea katika wadi ya Puma, eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale Rai amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya hali ya anga tatizo la njaa linaendelea kushuhudiwa kwa muda mrefu sasa.

Wakati huo huo Rai ametoa wito kwa vijana katika eneo la Kwale kukumbatia maswala ya uchumi samawati.

Akisema kuwa ni sekta muhimu itakayokuza vijana haswa ikizingatiwa kuwa waziri husika katika sekta hiyo anatoka kaunti ya Kwale.

BY NEWS DESK