HabariNews

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamepinga vikali kufungwa kwa Mangwe.

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamepinga vikali pendekezo la idara ya usalama ya kutaka kuzifunga sehemu za uuzaji wa pombe ya mnazi almaarufu Mangwe.

Wakiongozwa na Ramba Mwakigato, wakaazi hao wamekanusha madai kuwa sehemu hizo zinachangia pakubwa kudorora kwa usalama katika kaunti hiyo.

Wakaazi hao pia wametaja utumizi wa mnazi kuwa salama kwa afya ya binadamu ikizingatiwa kwamba ni pombe ya kienyeji.

Kwa upande wake kamishna wa Kwale Gideon Oyagi ametishia kuzifunga mangwe zinazotumika kupanga mikakati ya utekelezaji wa visa vya uhalifu.

Hata hivyo, Oyagi amewataka wauzaji wa mnazi kuzingatia sheria zilizowekwa ili kuhakikisha kuwa biashara zao zinaendelea bila changamoto yoyote.

BY EDOTORIAL TEAM