HabariNews

Salim Mvurya awataka mawaziri wa kaunti ya Kwale walioapishwa kufanya kazi kwa kushirikiana na gavana wa kaunti hiyo.

Waziri wa madini na uchumi samawati Salim Mvurya amewataka mawaziri wa kaunti ya Kwale walioapishwa kufanya kazi kwa kushirikiana na gavana wa kaunti ya Kwale ili kufanikisha ajenda za maendeleo walizoahidi wakaazi wa Kwale.

Mvurya amekariri kuwa ni kupitia ushirikiano mzuri ambapo kaunti ya Kwale itakuwa kielelezo kwa kaunti zingine nchini.

Ni kauli iliyoungwa mkono na Gavana wa Kwale Fatuma Achani ambapo amewasihi mawaziri hao kufanya kazi kikamilifu sawia na kuchukua majukumu yao kikamilifu akisistiza kuwa ni kupitia ushirikiano mzuri baina ya viongozi kwale utakaoleta maendeleo.

Haya yanajiri huku mawaziri wanane wakiapishwa baada ya wawili kukataliwa kutokana na kutofikia viwango hitajika.

Wakati huo huo Mvurya amewaonya vikali wafanyibiashara wa sekta hiyo dhidi ya kuendeleza shughuli ya uchimbaji madini kinyume na sheria.

Amesema kuwa wafanyibiashara watakaopatikana watafungiwa sehemu zao za kuchimba madini akiongeza kuwa sehemu hizo ambazo hazina leseni ya kuhudumu kulingana na sheria zilizowekwa na serikali zitafungwa.

Aidha amesisitiza kuwa marufuku ya uchimbaji madini yaliyowekwa na serikali katika eneo la Kuranze huko Kinango yangali yanaendelea.

Mvurya amewataka wafanyibiashara wa eneo hilo kujisajili upya kwenye mtandao ili kupata leseni ya madini.

BY EDITORIAL TEAM