HabariNews

KERO LA NDOVU WADI YA MWERENI.

Wakaazi katika kijiji cha Kasemeni , wadi ya Mwereni eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale wanalalamika kuhusu uhaba wa maji katika mabwawa madogo ya eneo hilo baada ya ndovu kunywa yote.

Kulingana na Beatrice Mwikali ndovu wamekuwa wakizunguka katika kijiji hicho na kumaliza maji huku wakiendelea kushuhudia uhaba huo kwa muda mrefu sasa.

Mwikali akisema kuwa kwa sasa hawawezi kuendelea hata na shughuli za ukulima kutokana na kukauka kwa maji hayo akiongeza kuwa imewabidi wanaume katika kijiji hicho kulala katika mabwawa hayo kulinda ili wanayama pori wasiyanywe.

Akisema kuwa ni jambo ambalo linawatatiza maisha na hata kuhatarisha maisha yao.

Wakiitaka serikali kuja na suluhu ya ndovu hao ambao kwa wamekuwa kero.

BU EDITORIAL DESK