HabariNews

Wakaazi wa Kwale wahakikishiwa usalama msimu huu wa sherehe za mwaka mpya,

Kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amewahakikishia usalama wa kutosha wakaazi pamoja na wageni wanaopania kusheherekea sikukuu ya mwaka mpya.

Akizungumza huko mjini Kwale, Oyagi amewataka wenyeji pamoja na wageni kutohofu kuhusu usalama wao wakati wa mkesha wa sherehe za mwaka mpya.

Kamishna huyo amedokeza kuwa tayari idara ya usalama imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuna mazingira bora kwa wale watakaosherekea usiku wa mwaka mpya.

Wakati uo huo, Oyagi amesema kuwa maafisa wa usalama watakuwa macho kukabiliana na wahalifu wanaowahangaisha raia nyakati za usiku.

Kamishna huyo ameonya kwamba watakaopatikana wakivuruga amani ya kaunti hiyo wakati wa sikukuu watachukuliwa hatua kali za kisheria.

BY EDITORIAL DESK