Wakaazi katika kijiji cha Ndavaya , Kinango kaunti ya Kwale wanakadiria hasara ya chakula chao baada ya mahindi waliyopanda kuharibiwa na viwavi jeshi.
Kulingana na Fatuma Nyawawi kwa sasa hana chakula baada ya viwavi hao kuharibu mahindi katika shamba lake, akisema kuwa wadudu hao walianza kuvamia shamba lake tangu mwezi Novemba mwaka jana na kumaliza kila kitu akiendelea kutaabika na njaa.
Vilevile ameongeza kuwa hakuna msaada wa kuondoa wadudu hao hadi kufikia sasa na hofu ya njaa inazidi kumkodolea macho.
Ameitaka serikali kumsaidia kumaliza wadudu hao na pia kupata chakula kwani ukosefu wa kuvuna mahindi umewasabibishia njaa.
BY EDITORIAL DESK