HabariNewsSiasa

Gavana wa Kwale Fatuma Achani awaonya makatibu katika kaunti kwa kuchukua zabuni ambazo zinastahili kupewa wakaazi.

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amewaonya makatibu katika kaunti kwa kile kilichodaiwa kuwa baadhi yao wamechukua zabuni ambazo zinastahili kupewa wakaazi ili waweze kujiinua kimaendeleo.

Achani aliyekuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Kwale amewataka mawaziri wa kaunti hio kuhakikisha kuwa hakuna ubaguzi wowote unaofanyika akisema kuwa ni jukumu la serikali ya kaunti kutoa nafasi za ajira kwa vijana.

 

Hata hivyo ameaahidi kufanya uchunguzi wa zabuni zinazotolewa pamoja na wenye kampuni huku akiwarai makatibu kutoa nafasi kwa wakaazi wa Kwale kufaidika na zabuni hizo.

 

Kauli yake inajiri baada ya baadhi ya makatibu kudaiwa kuchukua baadhi ya Zabuni licha ya wao kuwa serikalini hatua aliyoitaja unyanyasaji wa wananchi.

BY EDITORIAL DESK