HabariNews

Idara ya afya kwa ushirikiano na washikadau wengine imeweka mikakati mbali mbali ya kukabiliana na kiangazi.

Katika juhudi za kukabiliana na kiangazi na kuhakikisha kuwa watoto wanapata lishe bora katika kaunti ya Kwale , idara ya afya kwa ushirikiano na washikadau wengine imeweka mikakati mbali mbali kuona kuwa hali hiyo inakabiliwa.

Afisa mkuu wa lishe bora katika kaunti ya Kwale Rachel Kahindi amesema kuwa miongoni mwa mipango wanayoipigia upato ni ule wa kupeana fedha kwa familia ambazo zina watoto wachanga kando na kuwapa chakula.

Kahindi ameongeza kuwa pia wanashirikiana na idara ya maji kuona kuwa usambazaji maji safi katika maeneo kame inaimarishwa.

Akisisitiza kuwa ukosefu wa maji safi huchagia ongezeko la magonjwa hivyo na kuathiri afya za watoto ata zaidi.

BY EDITORIAL DESK