HabariNews

Wanafunzi 16 waliokamilisha darasa la 8 mwaka jana wafaidika na ufadhili wa masomo wa Wings to fly.

Jumla ya wanafunzi 16 waliokamilisha darasa la 8 mwaka jana kaunti ya Kwale ni miongoni mwa wanafunzi 1000 nchini waliofaidika na ufadhili wa masomo wa Wings to fly kutoka kwa usimamizi wa benk ya Equity mwaka huu.

Jacob Akida mkurugenzi wa benki hio tawi la Kwale amesema kwamba wanafunzi hao waliopata zaidi ya alama 350 wanatoka katika familia zisizojiweza .

Amewataka wazazi ambao watoto wao wamefaidika na mradi huo kuwapatia ushauri mwafaka wanapojiandaa kujiunga na shule za upili ili kuona kwamba wanajitenga na visa vinavyolenga kutatiza masomo yao.

 

Wanafunzi hao wanatarajiwa kujumuika  na wanafunzi wengine  waliopata  ufadhili  huo humu nchini ili kupata ushauri mwafaka kuhusiana na maswala ya elimu  kwa muda wa siku 3 katika shule ya upili ya wasichana ya kitaifa ya Pangani.

BY EDITORIAL DESK