HabariNews

Wizara ya maswala ya kigeni nchini kutathimini viwanda na kampuni vinavyomilikiwa na waekezaji wa nchi za kigeni.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini imeanzisha mchakato wa kutathimini viwanda na kampuni zinavyomilikiwa na waekezaji wa nchi za kigeni ili kuona jinsi itakavyoboresha miundo msingi ili kuhakikisha Mazingira salama kwa wafanyikazi.

Waziri wa maswala ya kigeni Dr.Alfred Mutua anasema kwamba baadhi ya kampuni zimekosa ufuatilizi mzuri kutoka kwa serikali hatua inayopelekea kukumbwa na changamoto nyingi za kimsingi hatua inayopelekea kusambaratika kimapato.

Aidha ametaja kampuni na viwanda kuwa na mchango mkubwa wa ajira humu nchini.

Ameyasema haya katika kiwanda cha kusaga nazi cha Kentaste chini ya usimamizi wa mwekezaji kutoka taifa la Canada kilichoko huko diani kaunti ya Kwale.

BY NEWS DESK