HabariNews

Benki ya HFC na chuo kikuu cha Strathmore zatangaza kushirikiana kuwezesha biashara ndogondogo.

Kampuni tanzu ya benki ya HFC na chuo kikuu cha kibiashara cha Strathmore zimetangaza kushirikiana
katika mpango wa uwezeshaji wa biashara ndogondogo na kati ndani ya sekta ya viwanda, uuzaji wa
nyumba, huduma za afya, elimu na kilimo.

Chini ya mpango huo ,washirika watanufaika katika mafunzo, ushauri wa biashara, kujijenga na hata
kupata suluhisho la kifedha ambalo linalenga ukuaji wa biashara.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya HF Robert Kibaara anasema kuwa biashara ndogondogo na za kati,
ndio zimekuwa shina la Maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiviwanda ya Kenya.

Kwa ushirikiano na bank hii pamoja na chuo cha Strathmore, tutashirikiana kwa ujuzi wakila mmoja,kwa
kuja na mbinu zitakazowezesha biashara hizi ili kuwa kiungo muhimu zaidi cha maendeleo ya taifa hili,’’
Aliongeza Mkurugenzi Robert Kibaara.

Kwa upande wake afisaa mkuu wa wanafunzi katika chuo cha kikuu cha Strathmore Caesar Mwangi,
biashara ndogondogo zinajumuisha asilimia 98 ya biashara zote nchini huku zikizalisha asilimia 30 kila
mwaka pamoja na kuchangia asilia 3 ya pato la kitaifa.

Kulingana na ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu nchini ya 2018 inaonesha kuwa takriban biashara laki 4
ndogo ndogo na zile za kati hafiki mwaka wa pili huku chache zilizosalia hazidumu kwa miaka 5.

BY EDITORIAL DESK