HabariLifestyleNews

Kampuni DT Dobie yatangaza bidhaa mpya sokoni.

ampuni ya kutangeneza magari ya DT Dobie imetangaza bidhaa yake mpya ya gari aina ya Lori la kubeba mizigo.

Hii ni baada ya kushirikiana na kampuni ya utengenezaji magari ya uchina ya Sinotruck ambayo tayari imeweka matawi yake sehemu tofauti hapa nchini.

Malori hayo ya HOWO yanalenga kusaidia pakubwa katika sekta ya kibiashara hasa usafirishaji mizigo hapa nchini na hata afrika mashariki.

Mkurugenzi katika kampuni hiyo James Bon amesema pia waneshirikiana na taasisi za kifedha ili kufanikisha upatikanaji wa haraka wa mikopo Kwa wateja wake.